KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, September 29, 2011

TEVEZ APIGWA STOP ETIHAD STADIUM.

Uongozi wa klabu ya Man City umemsimamisha kwa muda wa majuma mawili mshambuliaji kutoka nchini Argentina Carlos Tevez kufuatia utovu wa nidhamu aliouonyesha katika mchezo dhidi ya Fc Bayern Munich usiku wa kuamkia jana huko Allianze Arena.

Uongozi wa klabu hiyo ya Etihad Stadium umefikia maamuzi hayo baada ya kupoa taarifa kamili kutoka kwa meneja Roberto Mancini ambae alikiri kuchukizwa na tabia aliyoonyeshwa na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

Taarifa iliyotolewa imeeleza kwamba kwa kipindi cha majuma mawili, uchunguzi utafanyika wa kubaini nini chanzo kilichopelekea Caros Tevez kugoma kuingia uwanjani kama mchezaji wa akiba wakati tayari Bayern Munich walikua wanaongoza mabao mawili kwa sifuri yaliyofungwa na Mario Gomes.

Taarifa hio imeongeza kwamba Carlos Tevez akiwa anaendelea na adhabu hiyo hatoruhusiwa kufanya shughuli yoyote klabuni hapo pamoja na kujumuika na wachezaji wenzake watakapokua mazoezini.

Hata hivyo Roberto Mancini ameshatoa msimamo wake wa kutokua tayari kushirikiana na mchezaji huyo mpaka hapo mkataba wake utakapofikia kikomo ama kuondoka kama mchezaji atakaeuzwa kwenye klabu nyingine itakayokua tayari kumsajili.

Kama itakumbukwa vyema Carlos Tevez alitoa kauli yake mara baada ya kurejea nchini Uingereza wakitokea nchini Ujerumania mbapo alisema kuwa benchi la ufundi lilimuelewa vibaya kufuatia maamuzi aliyoyafanya, lakini akaahidi atakuwa tayari kufanya chochote atakachoagizwa kukifanya klabuni hapo.

No comments:

Post a Comment