KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 21, 2011

HISPANIA WAREJEA KILELENI.

Mwezi mmoja baada ya kushuka katika viwango vya ubora wa soka duniani na kukamata nafasi ya pili, mabingwa wa dunia pamoja na barani Ulaya Hispania, wamerejea katika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya viwango hivyo ambayo ilikua ikiongozwa na washindi wa pili katika fainali za kombe la dunia Uholanzi.

Uholanzi na Hispania wamepishana katika nafasi hizo, kufuatia vigezo tofauti kutumiwa na shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA baada ya kuonekana mataifa hayo mawili yaliibuka na ushindi katika michezo ya kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2012 iliyochezwa mwanzoni mwa mwezi huu.

Kigezo kilichotumika katika uwiyano wa kuzipishanisha nchi hizo katika viwango vya ubora duniani ni fainali za kombe la dunia za mwaka 2010 pamoja na fainali za mataifa ya Ulaya za mwaka 2008, ambapo Hispania imeonekana kuwa na sababu ya kurejea kileleni kutokana na matokeo mazuri waliyoyapata katika michuano hiyo.

Kwa kigezo hicho kilichotumika, nchi ya Uingereza ambayo ilijipatia ushindi katika michezo miwili ya kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Ulaya dhidi ya Bulgaria pamoja na Wales mwanzoni mwa mwezi huu imeporomoka kutoka katika nafasi ya nne hadi katika nafasi ya nane, baada ya kukosa nafasi ya kushiriki fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2008.

Nchi ya Ujerumani imeendelea kukamata nafasi ya tatu, huku mabingwa wa soka wa ukanda wa Amerika ya kusini Uruguay wakipanda kwa nafasi moja kutoka nafasi ya tano hadi ya nne na nchi ya Ureno imepanda kwa nafasi tatu kutoka katika nafasi ya nane hadi ya tano.

Katika hatua nyingine nchi zilizopo kwenye 50 bora ambazo zimeonyesha kupanda kwa kiasi kikubwa ni Uswiz ambayo imepanda kwa nafasi 12 ambapo imetoka katika nafasi ya 36 hadi nafasi ya 18, Bosnia-Herzegovina imepanda kwa nafasi 17 ambapo imetoka katika nafasi ya 39 hadi nafasi ya 22, Hungary imepanda kwa nafasi 18 ambapo imetoka katika nafasi ya 45 hadi nafasi ya 27 na nchi ya Armenia imeingi katika kundi hili baada ya kupanda nafasi 27 ikitoka katika nafasi ya 71 na sasa inakamata nafasi ya 44.

Kumi bora ya viwango vya ubora wa soka ulimwenguni vilivyotolewa hii leo inaonekana kwamba:

1 from 2. Spain 1605 points

2 from 1. Holland 1571pts

3. Germany 1290

4 from 5. Uruguay 1184

5 from 8. Portugal 1158

6 from 7. Italy 1142

7 from 6. Brazil 1132

8 from 4. England 1089

9 from 10. Croatia 1057

10 from 9. Argentina 1024.

No comments:

Post a Comment