KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 21, 2011

Gian Piero Gasperini AONYESHWA MLANGO WA KUTOKEA.

Klabu bingwa duniani Inter Milan imekua klabu ya kwanza katika ligi ya nchini Italia kumtimua meneja wake baada ya mambo kuwaendea kombo toka mwanzoni mwa msimu huu.

Inter Milan wametangaza kumtimua kazi Gian Piero Gasperini ikiwa ni siku moja baada ya matokeo ya kusikitisha ya mabao matatu kwa moja yalioyowaacha mabingwa hao wa dunia mikoni mitupu huku point tatu muhimu zikielekea kwa wapinzani wao Novara.

Taarifa za kutimuliwa kazi kwa meneja huyo kutoka nchini Italia ambae kabla ya kujiunga na Inter Milan alikua akiitumikia klabu ya Genoa, zilithibitishwa mapema hii leo asubuhi kabla ya kuanza kwa mazoezi ambayo yaliongozwa na mameneja wasaidizi Daniele Bernazzani pamoja na Giuseppe Baresi.

Mara baada ya mchezo wa jana usiku, raisi wa klabu ya Inter Milan Massimo Morati alinukuliwa na vyombo vya habari akisema Gian Piero Gasperini ameshindwa kukiweka sawa kikosi chake na anaamini huenda timu imemshinda uwezo.

Hata hivyo alipohojiwa meneja huyo alisema bado ana matumaini ya kufanya vizuri kutokana maelewano mazuri yaliopo kati yake ya wachezaji wote kikosini ambao mpaka usiku wa kuamki hii leo walikua wameshapoteza michezo mitatu ya ligi pamoja na mchezo mmoja wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Trabzonspor kutoka nchini Uturuki.

Mpaka sasa bado haijathibitishwa ni meneja yupi atakaemrithi Gian Piero Gasperini, huku kikosi cha Inter Milan kikiendelea na maandalizi ya mchezo wa mwishoni mwa juma hili katika michuano ya ligi ya nchini Italia dhidi ya Bologna na kisha mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya CSKA Moscow utakaochezwa nchini Urusi kati kati ya juma lijlo.

No comments:

Post a Comment