KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 27, 2011

Huub Stevens MENEJA MPYA WA SCHALKE 04.

Wana nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu uliopita, Schalke 04 wamemteua Huub Stevens kuwa meneja wa klabu hiyo baada ya Ralf Rangnick alietangaza kujiuzulu mwishoni mwa juma lililopita kufuatuia sababu za kiafya.

Huub Stevens ambae ni raia kutoka nchini Uholanzi ameteuliwa kushika wadhifa huo huku akikumbukwa na wengi kufautia mchango wake alioutoa huko Veltins-Arena, mjini Gelsenkirchen ambao ulipelekea kuizawadia ubingwa wa kombe la UEFA klabu ya Schalke 04 mwaka 1997 pamoja na ubingwa wa kombe la nchini ujerumani mwaka 2001 na 2002 huku akiisaidia klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya Bundesliga katika msimu wa mwaka 2000-01.

Meneja huyo alieanza kazi ya kukinoa kikosi cha klabu Schalke kuanzia mwaka 1996 hadi mwaka 2002, amesaini mkataba wa miaka miwili ambao utafikia kikomo mwezi June mwaka 2013.

Mapema hii leo alitarajiwa kuanza kibarua cha kukinoa kikosi chake tayari kwa mchezo wa ligi ya barani Ulaya dhidi ya Maccabi Haifa utakaochezwa siku ya Al-khamis na kisha mchezo wa ligi wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Hamburger SV.

Stevens, ambae kwa sasa bado anaendelea kushikilia rekidi ya kipekee ya kuizawadia mafanikio makubwa Schalke 04, pia aliwahi kuzinoa klabu za nchini Ujerumani kama FC Cologne, Hamburg SV pamoja na Hertha Berlin.

Kwa upande wa nchini kwao Uholanzi meneja huyo mwenye umri wa miaka 57 amewahi kuinoa klabu ya PSV Eindhoven pamoja na RB Salzburg ya nchini Austria.

No comments:

Post a Comment