KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 27, 2011

Jack Wilshere AFANYIWA UPASUAJI KWA USALAMA.

Kiungo kutoka nchini Uingereza Jack Wilshere huenda ikamchukua muda wa miazi sita kurejea tena uwanjani, baada ya kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu kwa mafanikio makubwa hapo jana.

Jack Wilshere ambae bado hajacheza mchezo wowote wa ligi ya nchini Uingereza msimu huu anapewa nafasi ya kurejea uwanjani kwa kipindi hicho huku ikiaminiwa hatua hiyo itampa munkari wa kucheza kwa kujituma ipasavyo.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19, amesema ni hatua nzuri kwake kufanyiwa upasuaji kwa mafanikio makubwa na anaamini kila jambo lililo mbele yake litafanikiwa pia kutokana na kutarajia kurejea uwanjani akiwa katika mtazamo tofauti.

Amesema ni wakati mgumu sana kwake kwa hivi sasa kwani alitamani kurejea uwanjani kusaidiana na wengine kwa lengo la kuhakikisha klabu yao inafanya vizuri baada ya kuanza vibaya lakini bado akaendelea kubainisha kuwa anaamini waliosalia kikosini wataifanya kazi hiyo.

Hata hivyo amewashukuri mashabiki wake pamoja na wale wa klabu ya Arsenal kwa salamu za pole walizomtumia kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twiter, hatua ambayo ameichukulia kama sehemu ya kuwa pamoja na mashabiki hao katika kipindi hiki cha kujiuguza.

Jack Wilshere, aliumia kifundo cha mguu katika mchezo wa kuwania kombe la Emirates mwanzoni mwa msimu huu, na ilidhania huenda angerejea uwanjani mapema lakini mambo yalikwenda tofauti na kupelekea kufanyiwa upasuaji hapo jana.

Wakati huo kikosi cha Arsenal kesho kitashuka dimbani bila ya kuwa na wachezaji watatu ambao ni majeruhi.

Wachezaji hao ambao hawatokuwepo kikosini hiyo kesho ni Laurent Koscielny, Theo Walcott pamoja na Gervais Yao Kouassi Gervinho.

Laurent Koscielny anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu, Gervinho anasumbuliwa na maumivu ya misuli huku Walcott akiendelea kuuguza maumivu ya goti aliyoyapata mwishoni mwa juma lililopita wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya Bolton Wanderers.

Hata hivyo wachezaji hao wanapewa nafasi kubwa ya kucheza mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo Arsenal watakuwa ugenini wakicheza na Tottenham Hotspur.

Kesho Arsenal watakuwa na mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Olympiacos kutoka nchini ugiriki.

No comments:

Post a Comment