KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 23, 2011

King Kenny Dalglish ATOA MSIMAMO WA LIVERPOOL.

Meneja wa majogoo wa jiji Liverpool King Kenny Dalglish amesema hakuna mchezaji kati ya wachezaji walio chini yake ambae ana mamlaka zaidi ya klabu hiyo yenye historia ya kipekee katika soka la nchini uingereza na barani ulaya kwa ujumla.

King Kenny Dalglish ametoa msimamo huo baada ya kuchukizwa na kitendo cha mshambuliaji ghali aliesajiliwa na klabu hiyo akitokea Newcastle Utd mwanzoni mwa mwaka huu Andy Carroll cha kuondoka katika benchi katika mchezo wa hatua ya tatu ya kombe la ligi dhidi ya Brighton and Hove Albion uliochezwa usiku wa kuamkia jana.

Amesema kitendo cha mshambuliaji huyo hakukipenda na anadhani kilitokana na hatua ya kuchukizwa na mpango wa kutokujumuishwa kikosini hali ambayo amesema inastahili kuzoewa na kila mmoja kwani yeye kama meneja ana mamlaka ya kumuamuru nani akacheze uwanjani tena na katika mchezo gani.

Hata hivyo meneja huyo hakueleza ni adhabu gani itamuangukia mshambuliaji huyo aliesajiliwa na Liverpool kwa ada ya uhamisho wa paund million 35.

Katika hatua nyingine King Kenny Dalglish amesema kurejea kwa kiungo na nahodha wa kikosi chake Steven Gerrard amekuchukulia kama sehemu ya kufunguliwa kwa ukurasa mwingine klabuni hapo hasa ikizingatiwa tayari wameshapoteza michezo miwili ya ligi.

Amesema uwepo wa kiungo huyo kikosini utaleta taswira tofauti kwa wachezaji wengine kutokana na hasama ambayo amekua akiitoa pale mambo yanapokwenda tofauti na matarajio yao.

Pia Dalglish akasifia uwezo wa kiungo mshambuliaji kutoka nchini Wales Craig Bellamy, ambae usiku wa kuamikia jana alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza baada ya kusajiliwa kwa mara nyingine klabuni hapo akitokea Man City.

Liverpool kesho watakua nyumbani katika uwanja wa Anfiled wakiwakaribisha Wolves Hampton wanderers katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ambayo pia itashuhudia michezo mingine ikirindima katika viwanja vingine tofauti ambapo:

Etihad Stadium, Manchester
Manchester City v Everton

St. James' Park, Newcastle
Newcastle United v Blackburn Rovers

DW Stadium, Wigan
Wigan Athletic v Tottenham Hotspur

Anfield, Liverpool
Liverpool v Wolverhampton Wanderers

Stamford Bridge, London
Chelsea v Swansea City

Emirates Stadium, London
Arsenal v Bolton Wanderers

The Hawthorns, West Bromwich
West Bromwich Albion v Fulham

Britannia Stadium, Stoke-on-Trent
Stoke City v Manchester United

No comments:

Post a Comment