KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 23, 2011

Owen Coyle AITABIRIA MEMA ARSENAL.

Katika harakati za kuelekea mchezo wa kesho kati ya washika bunduki wa Ashburton Grove Arsenal dhidi ya Bolton Wanderers, Owen Coyle ameitabiria mema The Gunnes kwa kusema anaamini klabu hiyo itamaliza katika nafasi nne za juu licha ya kuanza vibaya msimu huu wa ligi kwa kupoteza michezo mitatu, kupata ushindi mmoja na kutoka sare mara mopja.

Owen Coyle ambae ni meneja wa Bolton Wandereres amesema Arsenal bado ni klabu kubwa na yenye kila sababu ya kutimiza malengo hayo na mpaka sasa hajashangazwa na juhudi zinazofanya na meneja Arsene Wenger kuhakikisha mipango ya kurejea katika makali inakamilika.

Amesema mashabiki wengi wa soka ulimwenguni kwa sasa wanaizungumza vibaya klabu hiyo kutokana na mazingira yaliopo, lakini ukweli ni kwamba bado kuna mtazamo tofauti anaouona wa The Gunners kumaliza katika nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi.

Akizungumzia mpambano wa hapo kesho ambapo Bolton Wanderers watasafiri hadi jijini London kucheza na Arsenal, Owen Coyle amesema amekiandaa vyema kikosi chake na anaamini kutokana na maandalizi hayo kutakuwepo na upinzani mkubwa.

Bolton Wanderers wanaelekea jijini London huku wakiwa na kumbu kumbu ya kupoteza mchezo wao wa ligi uliopita ambapo walikubali kufungwa nyumbani dhidi ya Norwich city walioibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Arsenal nao wataingia uwanjani hiyo kesho huku wakikumbuka kichapo cha mabao manne kwa matatu walichokipokea kutoka kwa Balckburn Rovers mwishoni mwa juma lililopita huko Ewood Park.

Katika historia Arsenal walipoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Bolton Wanderers wakiwa nyumbani mwaka 1962, na toka walipohamia katika uwanja wa Emirates hawajawahi kupoteza point dhidi ya The Trotters.

No comments:

Post a Comment