KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 5, 2011

LIGI YA ITALIA KUANZA IJUMAA WA WIKI HII.

Hatiamae mgomo uliofanywa na wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nchini humo umemalizwa hii leo baada ya chama cha wachezaji pamoja na wasimamizi wa ligi ya Sirie A kufikia makubaliano rasmi.

Mgomo huo uliodumu kwa majuma kadhaa sasa na kusababisha kuchelewa kuanza kwa ligi ya soka nchini Italia, umefikia tamati huku pande hizo mbili zikiridhishana ambapo sasa wachezaji watalipwa haki zao kama walivyokua wakizidai siku za nyuma.

Raisi wa kamati ya usimamizi wa ligi ya nchini Italia Maurizio Beretta amewaambia waandishi wa habari kwamba ni furaha kubwa sana kwao kumaliza matatizo yaliyokua yanawakabili na sasa wanachosubiri ni kuona ligi inaanza kuchezwa katika viwanja mbali mbali.

Kiongozi huyo amedai kwamba mkataba walioingia na chama cha wachezaji upo wazi kwa kila mmoja wao, na hadhani kama kutakua na malalamiko tena mpaka mwezi June mwaka 2012 ambapo itakua mwisho wa mkataba huo.

Nae raisi wa chama cha wachezaji nchini Italia Damiano Tommasi amesema kama uongozi wa kamati ya kusimamia ligi umedhihirisha wazi makubaliano waliyofikia hakuna haja ya kuzungumza kwa kina zaidi ya kushukuru kwa kila jambo lilivyokua likipangwa katika mikutano yao.

Kumalizika kwa mgomo huo, kunaifanya ligi ya nchini Italia kuanza kuunguruma siku ya ijumaa ambapo mabingwa watetezi AC Milan watafungua kwa kucheza na SS Lazio katika uwanja wa San siro.

No comments:

Post a Comment