KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 6, 2011

Maria Mutola AREJEA KATIKA SOKA.


Mwanariadha maarufu kutoka nchini Msumbiji ambae alietamba miaka ya 1990 hadi miaka ya 2000 kupitia mbio za miata 800 Maria Mutola, amerejea tena katika mchezo wa soka baada ya kucheza mchezo akiwa binti mdogo.

Mutola, anaejulikana kwa jina la Maputo Express, amesema baada ya kustaafu mchezo wa riadha, aliamua tena kurudi katika mchezo wa soka kwa ajili ya kuweka mwili wake katika afya nzuri, na pia kwa lengo la kujifurahisha.

Amesema amekuwa akicheza soka katika klabu ya Sundowns huko nchini Afrika Kusini, na sasa ameitikia wito baada ya kuitwa katika timu ya taifa ya wanawake ya Msumbiji ambayo inashiriki michuano ya barani Afrika inayoendelea mjini Maputo.

Amesema mchezo wa soka sio mpya kwake na kurejea tena katika mchezo huo ni sawa na mtu alierejea nyumbani kwa mafanikio makubwa.

Akiwa na umri mdogo, Maria Mutola alikuwa akicheza soka na wavulana, kutokana na wakati huo kulikua hakuna ligi wala timu za wanawake.

No comments:

Post a Comment