KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 26, 2011

Armand Traore NDANI YA KADHIA NZITO.

Meneja wa Queens Park Rangers Neil Warnock amemlaumu beki wa pembeni wa klabu hiyo Armand Traore kufuatia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo wa jana ambao uliwakutanisha na Aston villa huko Loftus road.

Neil Warnock amemlaumu beki huyoa liemsajili akitokea arsenal ya jijini London kwa kusema hakustahili kufanya kosa la kumchezea rafu Marc Albrighton wa Aston Villa, katika dakika za mwisho za mchezo huo na kupelekea kuonyeshwa kadi ya pili ya njano ambayo ilizaa kadi nyekundu.


Amesema licha ya umoja wa wachezaji waliosalia uwanjani kusaidia na kusawazisha bao na kufanya matokeo kuwa bao moja kwa moja, bado anafikiria kumtoza faini Armand Traore ili iwe fundisho kwake na kwa wachezaji wengine ambao wanastahili kujua umuhimu wao pele timu inapokua inahitaji ushindi.

Hata hivyo picha za televisheni zimeonyesha kwamba Armand Traore alikua na lengo la kutaka kumiliki mpira lakini kwa bahati mbaya alijikuta akishindwa kutimiza malengo hayo na kumchezea rafu Marc Albrighton.

Kwa mantiki hiyo sasa beki huyo kutoka nchini Ufaransa atakosa mchezo ujao wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza ambapo QPR watakua wageni wa Fulham huko Craven Cottege mwishoni mwa juma hili.

No comments:

Post a Comment