KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, September 26, 2011

VITUO VYA TELEVISHENI VINAHUSUDIWA KAMA MUNGU.

Majuma kadhaa baada ya kurejesha mahusino na shirika la utangazaji la nchini Uingereza BBC, meneja wa mabingwa wa soka nchini humo Man utd Sir Alex Ferguson amepasua ukweli kwa kusema vituo vya televisheni vinavyoonyesha soka barani Ulaya vimepewa udhibiti mkubwa kupita kiasi.

Sir Alex Ferguson ambae alikorofishana na shirika hilo la utangazaji la nchini Uingereza toka mwaka 2004, kufuatia taarifa za kashfa zilizotolewa dhidi ya mwanae wa kiume amepasua ukweli huo alipofanyiwa mahojiano na BBC ambapo amesema kutokana na muonekano wa udhibiti huo vilabu vimepoteza udhibiti wa ratiba, hali inayoathiri timu zinazocheza soka barani Ulaya.

Mzee huyo kutoka nchini Scotland amesema wahusika wa michuano mbali mbali barani ulaya, wamekua wakiviyhusudu sana vituo vya televisheni hatua ambayo inamfanya kuifananisha hali hiyo kama wanaadamu wanavyomuhusudu mwenyezi mungu.

Hata hivyo amedai kwamba, vilabu vya soka barani ulaya vinastahili kuamka na kushikamana kwa pamoja, kwa lengo la kudai haki ya kulipwa zaidi kutokana na mapato yanayotokana na kuonyeshwa kwa michezo inayowahusu.

Akitolea mfano kupitia ligi kuu ya soka nchini Uingereza, Sir Alex Ferguson amesema wasimamizi wa ligi hiyo tayari wameshauza haki ya kuonyesha michezo husika karibu katika nchi 200 duniani kote.

Amesema licha ya suala hilo kufahamika bado hawapewi fedha inayokidhi mipango iliyowekwa na wahusika wa ligi, kama wanavyotarajia wao.

Kama itakumbukwa vyema nchini Hispania, ligi ya nchini humo ilichelewa kuanza msimu huu, kufuatia mvutano ulioibuka kati ya vilabu na wasimamizi wa ligi hiyo, ambapo kubwa lilikua ni ulipwaji wa haki zinazotokana na kuonyeshwa kwa michezo kupitia televisheni.

No comments:

Post a Comment