KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 28, 2011

Mikel Arteta AMFAGILIA ARSENE WENGER.

Kiungo kutoka nchini Hispania Mikel Arteta amekiri kufurahia hatua ya kucheza michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mara baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza akiwa na klabu yake ya zamani ya Everton mwaka 2005 ambayo haikufika mbali baada ya kuondolewa katika hatua ya mtoano dhidi ya Villareal.

Mikel Arteta amesema ndoto zake kabla ya kujiunga na Arsenal mwanzoni mwa msimu huu, zilikua ni kucheza ligi hiyo na sasa anaamini ametimiza alichokua akikihitaji siku nyingi zilizopita.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 amesema kila mchezaji anaecheza soka barani Ulaya hutamani kucheza michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu, hivyo hana budi kukiri amefurahishwa na kitendo hicho.

Mikael Arteta usiku huu atacheza mchezo wake wa pili wa ligi ya mabingwa barani Ulaya akiwana kikosi cha Arsenal ambacho kitakua nyumbani kucheza na mabingwa wa soka toka nchini Uguriki Olympiacos mara baada ya kujumuishwa kikosini katika mchezo uliopita dhidi ya Borrusia Dotmund waliolazimisha matokeo ya sare ya bao moja kwa moja.

Ne meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesifiwa uwezo wa mchezaji huyo anapokua uwanjani ambapo amesema mikael arteta ana tabia ya kujituma wakati wote na hiyo ilikua sifa kubwa ya kumsajili akitokea Everton.

Wenger ameongeza kwamba aina ya uchezaji kama wa kiungo huyo amekua anavutiwa nao na anaamini usiku huu utakisaidia kikosi chake ambacho kinahitaji ushindi.

Arsene wenger usiku huu ataendelea kutumikia adhabu ya kutokukaa katika benchi aliyopewa na shirikisho la soka barani ulaya UEFA baada ya kudhidhirika alifanya mawasiliano na benchi hilo wakati wa mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano dhidi ya Udinese Calcio.

No comments:

Post a Comment