KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, September 28, 2011

Andre Villas-Boas APINGANA NA MASHABIKI.

Meneja wa klabu ya Chelsea Andre Villas-Boas ameahidi kuendelea kumpa nafasi ya kutosha kiungo kutoka nchini Uingereza Frank Lampard ambae kwa sasa anachukuliwa kwa mtazamo tofauti na mashabiki wa soka ulimwenguni kote kwa kudai kiwango chake kimeporomoka.

Andre Villas-Boas ametoa ahadi hiyo akiwa katika mkutano na waandihsi wa habari mjini Valencia nchini Hispania uliolenga kuzungumzia mpambano wa hii leo ambapo Chelsea watakua ugenini wakicheza na wenyeji wao Valencia CF huko Stadio Mestella.

Amesema yeye binafsi bado anaamini kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33, ana uwezo wa kutosha ambao utaendelea kuisaidia The Blues miaka kadhaa ijayo hivyo hayapi nafasi akilini mwake maneno yanayosemwa na mashabiki dhidi ya frank Lampard.

Amesema muda unavyozidi kwenda kiwango cha mchezaji huyo kinabadilika na anaamini ipo siku mashabiki wanaopinga suala hilo watakubaliana na yeye, kwa nini anaamua kuendelea kuwa na Frank Lampard kikosini.

Kikosi cha Chelsea usiklu huu kitakuwa huko Stadio Mestella, kwa lengo la kuendeleza mipango ya ushindi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri katika mchezo wa kwanza wa kundi la tano dhidi ya Bayer –Leverkusen majuma mawili yaliyopita.

Kiungo aliesajiliwa na Chelsea mwanzoni mwa msimu huu Juan Mata akitokea Valencia CF atakua miongini mwa wachezaji wanaotarajiwa kujumuishwa kikosini hatua ambayo inaaminiwa italeta upinzani wa hali ya juu kwa vikosi vya klabu hizo mbili.

No comments:

Post a Comment