
Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo zimeeleza kwamba beki huyo mwenye umri wa miaka 30 alikamatwa mapema hii leo na amefanyiwa mahojiano yanayohusianana tuhuma zinazomkabnili.
Titus Bramble anatuhumiwa kufanya vitendo hivyo usiku wa kuamkia hii leo hatua ambayo imewashangaza wengi kutokana na muonekano wake anapokua uwanjani.
Beki huyo alikua miongoni mwa wachezaji wa Sunderland waliocheza mchezo wa ligi kuu ya nchini Uingereza siku mbili zilizopita huko carrow road dhidi ya wenyeji Norwich city walioibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja.
Titus Bramble alianza kutambulika katika medani ya soka mara baada ya kupandishwa katika kikosi cha kwanza cha Ipswich town na baada ya hapo alisajiliwa na klabu ya Newcastel Utd kwa ada ya uhamisho wa paund million 5 mwaka 2002.

Mwezi uliopita mdogo wa Titus Bramble aitwae Tesfaye Bramble alihukumiwa kifungo cha miaka minne na nusu baada ya kukutwa na hatia ya kubaka.
Tesfaye Bramble mwenye umri wa miaka 19, hakupata nafasiya kufahamika vyema katika medani ya soka, kufuatia kucheza ligi za chini za nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment