
Hatua hiyo imeonekana kummkera mno meneja wa Man city Roberto Mancini ambapo amesema hatompa mshambuliaji huyo nafasi nyingine ya kucheza katika kikosi chake hadi hapo muda wa kuondoka Etihad Stadium utakapotimia.
Amesema hakufurahishwa na kitendo hicho cha Carlos Tevez ambae tayari alikua ameshamueleza taarifa za kumtumia kama mchezaji wa akiba lakini alipomuamuru ajiandae alimkatalia kata kata huku zikiwa zimesalia dakika 34 mpambano kumalizika.

Kwa upande wa Carlos Tevez mwenye umri wa miaka 27, amejitetea kwa kusema hakukataa kucheza katika mchezo huo wa jana na msimamo wake ulichukuliwa tofauti na meneja huyo kutoka nchini Italia.
Carlos Tevez pia amewataka radhi mashabiki wa Man city kwa kile kilichoonekana usiku wa kuamkia hii leo, huku akieleza wazi kwamba bado anaipenda klabu hiyo na atakua tayari kufanya atakachoelekezwa.

Katika mchezo huo wa kundi la kwanza wenyeji FC Bayern Munich walitimiza malengo yao ya kupata ushindi nyumbani, baada ya kuwabanjua wageni wao mabao mawili kwa sifuri yaliyofungwa na Mario Gomez katika dakika ya 38 na 45.
No comments:
Post a Comment