
Kiungo huyo ambae alijiunga na FC Barcelona mwezi August akitokea Arsenal ya nchini Uingereza, anakabiliwa na maumivu ya nyama za paja ambapo hatua hiyo inamfanya ajiunga na wachezaji wengine ambao ni majeruhi klabuni hapo kama Andres Iniesta, Alexis Sanchez pamoja na Ibrahim Afellay.
Kuumia kwake kunaendelea kumuumiza kichwa meneja wa Fc Barcelona Josep Pep Guardiola Isala, ambae alitarajia kumtumia katika mpambano wa kesho ambapo Barca watasafiri hadi huko Estadio El Molinón kupambana na wenyeji wao Sporting Gijon.
Cesc Fabregas , pia analazimika kuondolewa katika timu ya taifa ya Hispania baada ya kuitwa na kocha mkuu wa timu hiyo Vicente del Bosque kwa ajili ya mpambano wa mwishoni mwa juma lijalo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya dhidi ya jamuhuri ya Czech na kisha mchezo dhidi ya Scotland.
Mpaka sasa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, tayari ameshafunga mabao manne toka alipojiunga na Fc Barcelona akitokea Arsenal, hatua ambayo inaonyesha tayari ameshazoea mazingira ya huko camp Nou.
No comments:
Post a Comment