KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, October 3, 2011

Francesco Totti KUREJEA UWANJANI KATI KATI YA OKTOBA.

Nahodha na mshambuliaji wa Associazione Sportiva Roma Francesco Totti anapewa nafasi kubwa ya kucheza mchezo ujao wa ligi kuu ya soka nchini humo ambao utawakutanisha na mahasimu wao wakubwa wa mjini Roma Società Sportiva Lazio mnamo October 16.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35, aliumia misuli ya paja mwishoni mwa juma lililopita ambapo AR Roma walikua na kibarua cha kuwakabili Atalanta ambao walikubali kichapio cha mabao matatu kwa moja.

Francesco Totti anapewa nafasi ya kurejea uwanjani baada ya majuma mawili kupita, huku mashabiki wa SS Lazio wakimkumbuka kwa mabao yake mawili yaliyowazamisha katika mchezo wa ligi msimu uliopita uliochezwa mwezi wa tatu.

Totti hii leo amefanyia vipimo na jopo la mdaktari klabuni hapo na imethibitika hakuumia sana na sasa anatarajia kuanza mazoezi mepesi siku chache zijazo tayari kwa mchezo huo.

AS Roma pamoja na SS Lazio ambao wote kwa pamoja wanautumia uwanja wa Olympico kama uwanja wao wa nyumbani, wapo sawa katika msimamo wa ligi ya nchini Italia baada ya kufikisha point 8 lakini The Giallorossi *AS Roma* wapo katika nafasi ya sita kwa kuwa na tofauti nzuri ya mabao ya kufungwa na kufunga.

1 comment: