KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, October 3, 2011

Hamburg SV WAPO MSTUNI WAKISAKA MENEJA MPYA.

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Hamburg SV Frank Arnesen amesema klabu hiyo itakua chini ya meneja mpya mara baada ya kumalizika kwa wiki ya michezo ya kimataifa iliyoanza hii leo.

Frank Arnesen ametoa angalizo hilo, baada ya kikosi cha klabu hiyo inachoshiriki ligi kuu ya soka nchini Ujerumani, kuwa chini ya meneja wa muda Rodolfo Cardoso ambae amekua akiifanya kazi hiyo bila ya kuwa na sifa zinazohitajiwa na shirikisho la soka barani ulaya UEFA.

Rodolfo Cardoso ameifanya kazi hiyo kwa muda wa mwezi mmoja, na hii ilikuja baada ya kuondoka kwa meneja Michael Oenning alishindwa kutimiza malengo ya klabu.

Hata hivyo uongozi wa Hamburg SV ulikuwa umeshajipanga kufanya amzungumzo na Huub Stevens kwa ajili ya kumaliza tatizo la meneja klabuni hapo, lakini mpango huo ulikwenda tofauti baada ya kuwahiwa na viongozi wa Schalke 04 juma lililopita.

Lakini pamoja na mipango hiyo kuvurugika yasemekana uongozi wa Hamburg SV unajipanga kuzungumza na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Sergei Barbarez ambae ameonyesha nia ya kuwa tayari kuyavaa majukumu ya umeneja huko Imtech Arena.

1 comment: