
Harrison Afful amehimiza suala hilo la mshikamano na umoja huku akiutazama mchezo wa hapo kesho wa ligi ya mabingwa barani Afrika ambao utawakutanisha na Al Hilal ya nchini Sudan huko mjini Khartoum.
Beki huyo amesema kwa sasa kikosi chao kinaishikilia dhana hiyo na wanaamini itawasaidia kufanikisha suala la upatikananaji wa ushindi wakiwa katika uwanja wa ugenini.
Hata hivyo amekiri kwamba mpambano huo utakua mgumu kwa pande zote mbili lakini wao wameshajiandaa kukabiliana na hali yoyote watakayokutana nayo kutoka kwa Al Hilal ambao watakua na nguvu ya kushangiliwa na mashabiki wao wa nyumbani.
Amesema kwa muda wa juma zima wamekua na mazungumzo na uongozi wa benchi la ufundi kuhusiana na mpambano wa hapo kesho na suala kubwa linalosisitizwa ni ushirikiano na umoja.
Harrison Afful anatarajia kujumuishwa kikosini hiyo kesho baada ya kumaliza adhabu ya kuonyesha kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya mabingwa wa zamani wa barani Afrika Al-Ahly kutoka nchini ambao walilazimishwa sare wakiwa nyumbani.
No comments:
Post a Comment