KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, October 3, 2011

UONGOZI WA MAN CITY KUKUTANA NA TEVEZ.

Mshambuliaji kutoka nchini Argentina Carlos Tevez hii leo alitarajia kukutana na viongozi wa klabu ya Man city ikiwa ni sehemu ya kuendelea kwa uchunguzi unaofanya kufuatia tukio la kugoma kuingia uwanjani katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Fc Bayern Munich kati kati ya juma lililopita.

Tevez anakutana na uongozi wa klabu hiyo ya Etihad Stadium, huku akiwa anatumikia adhabu ya kufungiwa majuma mawili kufuatia tukio hilo ambalo lilipokelewa vibaya na wadau wa soka nchini Uingereza pamoja na huko nchini Ujerumani.

Sababu kubwa ya mkutano huo ni kutaka kufahamu upende wa Carlos Tevez ambao una haki ya kutetea kwa kile alichokifanya ambapo anadai hakukataa kuingia uwanjani kama ilivyoelezwa na meneja wa man city Roberto Mancini.

Katika moja ya taarifa za mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, alizozitoa mara baada ya kikosi cha Man city kuwasili mjini Manchester kikitokea nchini Ujerumani, ilieleza kwamba alikataa kufanya mazoezi ya kupasha mwili baada ya kutakiwa na Roberto Mancini kufanya hivyo kwa kuwa tayari alikua ameshapasha wakati wa mapumziko.

Endapo uongozi wa Man city utamkuta Carlos Teves na hatia juu ya tukio hilo huenda ukavunja makataba wake na kumuamuru aondokea Etihad Stadium akiwa kama mchezaji huru.

1 comment: