KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, October 1, 2011

VITA YA MANENO YA KUPAMBANA.

Meneja wa klabu ya Chelsea Andre Villas Boas amesema bado anakabiliwa na mazingira magumu ya kuzifahamu timu pinzani ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana nazo katika mchuano ya ligi kuu ya soka nchini uingereza.

Andre Villas Boas amezungumzia suala hili linalomkabili kwa sasa, kufuatia mchezo wa kesho dhidi ya Bolton Wanderers ambao atakutana nao kwa mara ya kwanza toka alipojiunga na The blues akitokea Fc Porto mapema mwezi wa saba.

Amesema ni vigumu kucheza na klabu usiyoifahamu vizuri, lakini akasema mipango aliyoikuta huko Stamford Bridge imekua ikimuongoza kuvifahamu vikosi vya wapinzani pale wanapokutana navyo.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 33, ameendelea kueleza kwamba mpambano wa kesho ambao utaunguruma huko Reebok Stadium utakua na sura tofauti kutokana na nafasi waliopo Bolton kwenye msimamo wa ligi ambapo watahitaji kujipapatua na kuondoka mkiani.

Pia amemzungumzia meneja wa Bolton Wanderers Owen Coyle ambae alipewa jukumu la kukonoa kikosi hicho mwaka 2010, kwa lengo la kuinusuru klabu hiyo iliyokua mkiani na kwa bahati nzuri alifanikiwa kufanya hivyo.

Nae meneja wa Bolton Wanderers Owen Coyle akazungumzo kwa upande wake ni vipi anavyomchukulia meneja wa Chelsea Andre Villas Boas ambae alipewa shughuli hiyo mara baada ya kutimuliwa kazi Carlo Michelangelo Ancheloti.

Amesema meneja huyo ni mzuri licha ya kuwa na umri mdogo na mara kadhaa amekua akifuatilia namna anavyokinoa kiklosi cha Chelsea ambacho anaamini kesho kitaonyesha upinzani mkubwa dhidi ya kikosi cha Bolton Wanderers.

No comments:

Post a Comment