
Washika bunduki hao wameshindwa kushinda kombe kwa miaka minne mfululizo na kufikia hatua ya baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo kumlaumu Wenger kushindwa kuwasajili wachezaji nyota watakaoiwezesha klabu hiyo kushinda mataji.
Hata hivyo Wenger amewataka mashabiki hao kuwa na imani na timu yao kwani ana matumaini na wachezaji wenye umri mdogo wanaweza kuiletea klabu hiyo mafanikio makubwa. 

Wenger amesema anashangazwa na lawama zinatolewa dhidi yake na baadhi ya mashabiki kuhusu matokeo ya jumla ya klabu hiyo msimu uliopita na anashangwa na jinsi ambavyo mashabiki hao wanashindwa kuangalia juhudi na matokeo yaliyopatikana msimu uliopita.
Amesema Matokeo ya klabu hiyo kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka jana sio mabaya kama ambavyo watu wengine wanavyofikiria na kuongeza kuwa ni kweli kutoshinda kombe inauma lakini matokeo ya msimu uliopita yamelaumiwa sana hasa ikizingatiwa kuwa tangu mwaka 2005 hawajashinda kombe lolote.
No comments:
Post a Comment