Saturday, August 8, 2009

MILANGO IWAZI KWA ASTON VILLA.

Meneja wa klabu ya ASTON VILLA Martin O'Neill amefungua milango wazi kwa kiungo wa klabu ya Real Madrid Wesley Sneijder kujiunga na klabu hiyo .

Hatma ya kiungo huyo wa kimataifa ipo mashakani baada ya Real Madrid kutumia kiasi kikubwa cha fedha kuwasajili wachezaji wapya katika kikosi hicho.

Meneja O'Neill amekiri kuwa klabu hiyo inawahitaji wachezaji kama Sneijder ili iweze kuwa kuwa miongoni mwa vilabu vinne bora kutokana na kuwa na kipaji cha hali ya juu.

Katika hatua nyingine klabu ya AC Milan imekubali kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uholanzi Klaas-Jan Huntelaar kwa mkataba wa miaka minne utakaogharimu Paundi milioni 12.8.



Huntler ambaye juma lijalo anatimiza umri wa miaka 26 ameamua kujiunga na klabu ya Milan licha ya kuhitajika katika klabu ya Tottenham.

Tangu ajiunga na Real amefunga mabao manane ambapo mara baada ya kusajiliwa kwa wachezaji Karim Benzema, Cristiano Ronaldo na Kaka ameonekana kuwa kama mchezaji wa akiba.




No comments:

Post a Comment