Tuesday, August 11, 2009

VIEIRA ATOA MSIMAMO.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Ufaransa na klabu ya Inter Milan Patrick Vieira amesema huenda akasalia Stadio Giuseppe Meazza, yalipo makao makuu ya klabu yake ya sasa.

Vieira ametoa msimamo huo kufuatia taarifa zilizopo sasa za yeye kuwa mbioni kurejea katika klabu yake ya zamani ya Arsenal.


Vieira, mwenye umri wa miaka 33, anahusishwa na taarifa hizo baada ya kuanza katika michezo kumi akiwa na kikosi cha Inter Milan msimu uliopita hali ambayo imemsababishia kuachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa ambapo hata hivyo hali hiyo huenda ikamuathiri na kuzikosa fainali za kombe la dunia za mwaka 2010 zitakazofanyika nchini Afrika kusini.


Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger tayari ameshathibitisha kuendelea na taratibu za kutaka kumrejesha kiungo huyo ambae alikuwa nahodha wa The Gunners miaka mitano iliyopita.


No comments:

Post a Comment