
Kiungo wa kimataifa wa jamuhuri ya Czech Republic Radoslav Kovac amefanikiwa kujiunga moja kwa moja na klabu ya West Ham Utd ya nchini Uingereza akitokea katika klabu ya Spartak Moscow ya nchini Urusi.
Taarifa zilizotolewa kwenye mtandao wa ligi kuu ya soka nchini Urusi zimeeleza kuwa Kovac amekamilisha uhamisho huo wa moja kwa moja hii leo.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 alisajiliwa kwa mkopo na klabu ya West Ham Utd katika mzunguuko wa pili wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu uliopita akitokea katika klabu yake ya zamani ya Spartak Moscow.
No comments:
Post a Comment