Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Newcastle United Andy Carroll ametozwa fainali ya paund 1,000 na mahakama ya mjini Newcastle baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga mtu mmoja katika klabu ya usiku.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amedaiwa kufanya tukio hilo Disemba 7 mwaka jana hatua ambayo ilimpelekea mtu huyo kuumia vibaya sehemu za kichwa chake na kukimbizwa haraka hospitali.
Andy Carroll alistahili kutozwa faini ya paund 2500 lakini kufuatia hatua ya kukubali kufanya kosa hilo, Mahakama iliamua kumpunguzia faini hiyo na kumtaka alipe kiasi cha paund 1000.
Hata hivyo mshambuliaji huyo wa klabu ya Newcastle Utd alipofikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza alikana shitaka hilo hatua ambayo ilimlazimu hakimu kuahirisha kesi na kwa mshangao mkubwa hii leo amekubali kufanya kosa hilo katika klabu ya Blu Bambu.
Kufuatia hatua hiyo ya kutozwa faini ya paund 1,000 Andy Carroll ameachiwa huru hali ambayo imeonekana kumfurahisha na kufikia hatua ya kusema kwamba kwa sasa atakua anaitumikia klabu yake ya Newcastle kwa amani zaidi.
No comments:
Post a Comment