KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, October 25, 2010

BABU AMPA 5 Samir Nasri.


Baada ya kuwafunda adabu matajiri wa jiji la Manchester, Man city kwa kuwatandika bakora tatu kwa sifuri, meneja wa klabu ya Arsenal Arsène Wenger amemwagia sifa kedekede kiungo Samir Nasri kwa kumuelezea amekomaa kiuchezeaji.

Arsène Wenger amemsifia kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 kufuatia kuonyesha kandanda safi katika pambano la jana ambalo lilishuhudia Samir Nasri akifungua mlango wa mabao katika uwanja wa City of Manchester.

Mzee huyo amesema mchezaji huyo siku hadi siku amekua akionyesha uwezo mkubwa kwa kusaidiana na wenzake anapokua uwanjani hali ambayo imekua ikimsaidia kufikisha malengo ya ushindi yanayohitajika huko Emirates.

Amesema licha ya kufungua mlango wa mabao yaliyopatikana katika mchezo wa jana pia Samir Nasri alisababisha bao la mwisho lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Denmark Nicklas Bendtner katika dsakika ya 88.

Wakati huo huo nahodha na kiungo wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas amewakata ngebe wale wote wanaoubeza ushindi wao wa mabao matatu kwa sifuri kwa kisingizio wameifunga Man cvity iliyokua pungufu baada ya beki wao Dedryck Boyata kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya tano.

Cesc Fabregas amesema licha ya wengi kuzungumza juu ya ushindi wao kwa sababu za Man City kuwa pungufu, bado amedai kikosi chao kilikua na uwezo wa kuibamiza klabu hiyo hata kama kikosi cha Roberto Mancini kingewasimamisha wachezaji 15.

Hata hivyo nahodha huyo ameonekana kuyapuuza maneno hayo ya mashabiki hao huku akidai kwa sasa wanaufikiria mchezo ujao wa kuwania ubingwa wa kombe la ligi utakaochezwa siku ya jumatano dhidi ya Newcastle Utd kwenye uwanja wa St James Park.

No comments:

Post a Comment