KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, October 26, 2010

CAPELLO AMPA UKWELI ROONEY.


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello amemtahadharisha mshambuliaji wa kimataifa wa nchi hiyo Wayne Rooney kuhakikisha anarejea katika kiwango chake cha kawaida la sivyo atamtema katika kikosi chake ambacho kinatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa mwezi ujao.

Capello ametoa tahadhari hiyo kwa Rooney, kufuatia mshambuliaji huyo kutokuwa katika kiwango chake kwa kipindi kirefu hali ambayo yasemekana imesababishwa na maisha yake binafsi.

Kocha huyo amesema endapo Wayne Rooney atashindwa kuthibitisha uwezo wake akiwa na kikosi cha klabu yake ya Man utd hatosita kumtema na kumteua mshambuliaji mwingine ambae atakuwa katika kiwango cha kuitwa kwenye timu ya taifa.

Fabio Capello amesema kwa kipindi kirefu amekua akiwafuatilia wachezaji wengi wanaocheza katika klabu za ligi kuu ya wamemvutia hivyo ametoa changamoto hiyo kwa Wayne Rooney ili aweze kuachana mawazo yanayomfanya kushindwa kucheza vizuri akiwa uwanjani.

No comments:

Post a Comment