Meneja wa klabu ya Newcastle Utd Chris Hughton amemtaka mshambuliaji wa kikosi chake Andy Carroll kutulia na kuitumikia vyema klabu hiyo baada ya kumaliza kesi iliyokua ikimsibu kwa kipindi kirefu.
Chris Hughton amesema anaamini kwa kipindi kirefu kilichopita mshambuliaji huyo alikua anashindwa kuonyesha umahiri wake akiwa uwanjani kwa asilimia 100 kutokana na kesi iliyokua ikimkabili mahakamani lakini sasa kesi hiyo imekwisha na hana budi kurejesha akili zake uwanjani.
Amesema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kabla ya kukabiliwa na kesi ya kupigana katika moja ya klabu za usiku huko jijini Newcastle alikua katika kiwango kizuri hali ambayo ilimpa nafasi ya kuifungia mabao klabuni hiyo ilipokua kwenye michuano ya ligi daraja la kwanza msimu uliopita.
Kesi ya Andy Carroll jana ilifikia kikomo katika mahakama ya mjini Newcastle kwa mchezaji huyo kutozwa faini ya paund 1000 baada ya kukiri kupigana na kumsababishia maumivu makali kichwani jamaa aliepigana nae ambae alikimbizwa hospitalini.
No comments:
Post a Comment