Kipa wa klabu ya Liverpool Pepe Reina amesema mashabiki wa klabu hiyo hawakustahili kumlaumu mshambuliaji Fernando Torres aliekua anakabiliwa na njaa ya upachikaji wa mabao kabla ya kufunga bao lake la kwanza mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Blackburn Rovers.
Pepe Reina amesema mashabiki wa klabu ya Liverpool kabla ya kumuangushia lawama mshambuliaji huyo walistahili kufikiria ni nani anaifanya klabu hiyo kuitwa Liverpool ambapo jibu la swali hilo lingekuja ni wachezaji na si Torres hivyo walistahili kukilaumu kikosi kizima.
Amesema kufuatia lawama alizokua akiangushiwa mshambuliaji huyo, yeye binafsi alikua anaumizwa na kitendo hicho kutokana na Torres kutokuwa na uwezo wa kuufuata mpira nyuma na kwenda moja kwa moja kufunga bali alistahili kuwezeshwa kufanya hivyo.
Hata hivyo Reina amewataka mashabiki hao kuacha kasumba ya kulaumu kabla ya kufikiria jambo wanalolilaumu bali wanatakiwa kujua nini mustakabali wa kutatuza tatizo ambalo mwishoni mwa juma hili lilionekana kumalizwa kwa ushindi wa mabao mawili kwa moja uliopatikana mbele ya Blackburn huku Torres akifunga bao la pili kwa kuwezeshwa.
No comments:
Post a Comment