KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, October 26, 2010

Lukasz Fabianski AWAKOSHA WADAU.


Kiungo wa zamani wa klabu ya Arsenal Ray Parlour amesema kipa wa sasa wa klabu hiyo Lukasz Fabianski anstahili kuwa chaguo la kwanza baada ya kuonyesha kiwango kizuri toka alipochukua nafasi ya kukaa golini majuma matatu yaliyopita.

Ray PARLOUR amesema kipa huyo wa kimataifa toka nchinio Poland ameojnyesha hali ya kujiamini anapokua langoni hatua mbayo kwake anaiona ndio silaha kubwa kwa mchezoji anaeitumikia nafasi hiyo.

Akitumia mfano wa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita ambapo Arsenal walimchapa Man City mabao matatu kwa sifuri gwiji huyo wa soka nchini Uingereza amesema Lukasz Fabianski alionyesha umahiri wake kwa kulinda vyema milingoti miwili na hadi mwisho wa mchezo huo.

Ray PARLOUR pia amemsifia kipa huyo kwa umahiri mkubwa aliouonyesha kwenye michezo miwili ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo katika mchezo dhidi ya FK Partizan Belgred Lukasz Fabianski aliikoa Arsenal kwa kupangua mkwaju wa penati huku pia akiendelea kufanya hivyo katika mchezo mwingine wa michuano hiyo dhidi ya Shakhtar Donetsk ya nchini Ukraine.

Kwa kipindi cha miezi kdhaa sasa mashabiki wa klabu ya Arsenal pamoja na uongozi wa klabu hiyo umekua katika mipango mizito ya kufikiria ni vipi tatizo la mlinda mlango litakavyomalivya huku wengine walkishauri ni bora kipa mbadala asajiliwe mwezi januari mwakani.

1 comment:

  1. shida ni nyie watu mnataka mambo ya ajabu.kwa shabiki anayefuatilia soka la arsenal vizuri huyu siku zote ni goalkeeper mzuri sana.

    ReplyDelete