Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Paraguay Roque Luis Santa Cruz Cantero bado ana ndoto za kutaka kuihama klabu yake ya Man City katika kipindi cha dirisha dogo la usajili mwezi januari mwaka 2011.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ameendelea kuwa msimamo wa kutaka kuondoka klabuni hapo kufuatia kuwa na maisha magumu ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha klabu hiyo hatua ambayo kwake anaiona kama udhalilishaji.
Roque Luis Santa Cruz Cantero amesema mara kadhaa amekua akijitahidi kumshawishi meneja Roberto Mancini anapokua mazoezini lakini bado nafasi imekua finyu ya kufikiriwa katika kikosi cha kwanza ama hata kuweka katika orodha ya wachezaji wa akiba.
Amesema hakuzoea maisha hayo na sasa inamlazimu kuanza kufikiria safari ya kuondoka klabuni hapo na kujiunga na klabu nyingine ambapo anaamini endapo atafanya hivyo nafasi ya kucheza kila juma itapatikana.
Roque Luis Santa Cruz Cantero alisajiliwa klabuni hapo na Mark Hughes akitokea Blackburn Rovers na katika usajili wa mwanzoni mwa msimu huu alikaribia kuondoka huko City Of Manchester kwa matarajio ya kujiunga na klabu ya SS Lazio lakini dili hilo lilivunjika dakika za mwisho tena akiwa tayari ameshafika huko nchini italia.
No comments:
Post a Comment