Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Croatia na klabu ya Bolton Wanderers Ivan Klasnic ameingia katika kashfa nzito baada ya kukamatwa na jeshi la polisi huko nchini Uingereza kwa tuhuma za ubakaji.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amshikiliwa na jeshi la polisi katika mji wa Manchester huku taarifa zikieleza kwamba kitendo hicho cha ubakaji alikifanya siku ya jumatatu suiku.
Ivan Klasnic anadaiwa kufanya kitendo hicho dhidi ya msichana ya msichana mwenye umri wa miaka 17 hatua ambayo huenda ikimfanya ahukumiwe kifungo cha gerezani endapo atakutwa na hatia mara baada ya kupandishwa kizimbani.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo baada ya kufanya kitendo hicho hakutiwa mikononi mwa jeshi la polisi mara moja kufuatia taarifa za uhalifu wake kushindwa kufikishwa kwa wahusika mapema.
Msemaji wa jeshi la polisi mjini Manchester amesema bado wanaendelea na uchunguzi wa kosa hilo la ubakaji na watakapomaliza hatua hiyo mtuhumiwa Ivan Klasnic atafikishwa mahakamani kujibutuhuma zitakazokua zikimkabili.
No comments:
Post a Comment