KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, October 28, 2010

KUKUMBUKA NYUMBANI NI MUHIMU.


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Paraguay Roque Santa Cruz amesema haziungi mkono taarifa zilizotolewa juu ya mshambuliaji mwenzake wa klabu ya Man City Carlos Tevez ambae inasemakana yu tayari kurejea nyumbani kwao nchini Argentina.

Roque Santa Cruz amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote na yeye anaamini mshambuliaji huyoa mbae kwa sasa yupo nyumbani kwao Argentina ataendelea kuuheshimu mkataba wake na klabu ya Man city kama unavyoainisha.

Amesema kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na moja ya chombo cha habari nchini Hispania zilidai kwamba mshambuliaji huyo kwa sasa anataka kurudi nyumbani kwa lengo la kutaka kuwa karibu na familia yake kwake yeye haoni kama ni tatizo kubwa hilo lakini ukweli ni kwamba CVarlos Teves ataendelea kuwepo huko city Of Manchester.

Amesema yeye binafsi nae husikia uchungu kuwa mbali na familia yake lakini hana namba ya kuiepuka hali hiyo hatua mbayo amedai inamuandama Teves lakini hadhani kama itampelekea kuaamua kuondoka na kurejea nyumbani kwao Argentina kucheza soka.

Wakati Roque Santa Cruz akipingana na taarifa zilizotolewa juu ya Carlos Teves, meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini nae amekanusha taarifa hizo na kusema mshambuliaji huyo amemuhakikishia kurudi baada ya kupewa ruhusa ya kwenda kuuguza majeraha akliyoyapata mwishoni mwa juma lililopita.

Roberto Mancini amesema anaamini kuwa licha ya teves kupewa ruhusa ya kwenya kuuguza majeraha yake pia atapata nafasi ya kukaa kwa pamoja na familia yake hatua ambayo anaamini itamfanya kucheza kwa amani atakaporejea klabuni hapo.

Wakati huo huo mshambuliaji Roque Santa Cruz ameendelea kuzungumzia hatua ya kukereka na utaratibu wa kunyimwa nafasi ya kucheza ambapo hadi sasa amejumuishwa kikosini mara moja toka msimu huu ulipoanza.

Amesema hali hiyo inampa wakati mgumu na kujihisi kama anadhalilishwa na ndio maana amekua akifikiria kuondoka klabuni hapo ili aweze kupata nafsi ya kucheza kila juma.

No comments:

Post a Comment