KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, October 28, 2010

PEPE REINA HAONDOKI NG'O !!!!


Meneja wa klabu ya Liverpool Roy Hodgson amewatahadharisha mashetani wekundu Man Utd kukaa mbali na kipa wake Jose Pepe Reina ambae asemekana asalandiwa na klabu hiyo jasiri nchini Uingereza.

Roy Hodgson ametoa tahadhari hiyo baada ya kuibuka kwa tetesi zinazodai kwamba Jose Pepe Reina huenda akawa kipa mbadala wa Edwin van der Sar ambae ameshatoa taarifa mwishoni mwa msimu huu atatundika daluga.

Akitoa tahadhari hiyo kupiti vyombo vya habari meneja huyo wa kimataifa toka nchini Uingereza amesema kipa huyo katu hatoondoka katika himaya yake kutokana na mkataba mnono alionao hivyo uongozi wa Man utd wanastahili kulisahau suala hilo.

Amesema endapo wataendelea na utaratibu wa kutaka kumsajili Jose Pepe Reina watakua wanapoteza muda wao ambao anaamini endapo watautumia vyema wanaweza kuhangaika na kumpata kipa mwingine ambae ataziba mwanya wa mholanzi Edwin van der Sar.

Jose Pepe Reina mwenye umri wa miaka 28 tayari ameshasaini mkataba wa miaka sita toka mwezi April mwaka huu.

No comments:

Post a Comment