Kampuni ya Venkys imejitokeza hadharani na kueleza wazi dhamira ya kutaka kuinunua klabu ya soka ya Blackburn Rovers inayoshiriki michuano ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza. itakapofika mwezi Novemba mwaka huu.
Kampuni hiyo kutoka nchini India ambayo itakua ya kwanza kuwekeza katika soka nchini Uingereza imedhamiria kufanya hivyo hadi kufikia mwezi Novemba mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa hii leo na mwenyekiti wa klabu ya Blackburn Rovers John Williams zimeelza kuwa tayari dalili za kampuni hiyo kuwekeza klabuni hapo zimeshaanza kuonekana kufuatia muendelezo wa vikao unaonendelea hivi sasa.
John Williams amesema kwa mara ya mwisho uopngozi wa kampuni hiyo ulio chini ya kiongozi wake Anuradha Desai ulikutana na uongozi wa sasa wa klabu hiyo na kukubalina kwamba manunuzi rasmi yatafanywa mwezi novemba mwaka huu hatua ambayo imepokelewa kwa mikoni miwili.
Akizungumzia hatua hiyo meneja wa klabu ya Blackburn Rovers Sam Allardyce amesema hatua hizo ni nzuri kwake pamoja na uongozi mzima kutokana na mustakabali wa klabu hiyo kuwa katika matarajio ya sura tofauti.
Amesema endapo harakati hizo zitakamilika katika wakati muafaka, upo uwezekano mkubwa kwa kikosi chake kuongezewa nguvu yakuwasajiliwa kwa wachezaji wengine wenye uwezo zaidi.
No comments:
Post a Comment