KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, December 17, 2010

Aaron Ramsey NDIE MWENYE JUKUMU LA KUSAMEHE.


Meneja wa klabu ya Arsenal Arsène Wenger amesema kiungo wa kimataifa toka nchini Wales Aaron Ramsey ni mtu pekee mwenye uwezo wa kumsamehe kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Stoke City Ryan Shawcross.

Wenger ametoa msimamo huo, wakati kikosi chake kikiwa kwenye matayarisho ya kuelekea kwenye mchezo wa kesho ambao utawakakutanisha na Stoke City huko Emirates ikiwa ni mara ya kwanza kwa klabu hizo kukutana baada ya Ryan Shawcross kumvunja mguu Aaron Ramsey mwanzoni mwa mwaka huu 2010.

Amesema jukumu lake kubwa kama meneja wa klabu ya Arsenal lilikua ni kuhakikisha kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19 anapata matibabu na kumfariji wakati wa kuguza jeraha lake sambamba na kuhakikisha anarejea vyema uwanjani kama ilivyokua zamani.

Arsene Wenger pia amedai Aaron Ramsey ni kijana alivuka umri wa miaka 18 hivyo litakua jambo la kipuuzi endapo masuala yanayomuhusu yakazungumzwa na mtu mwingine ili hali yeye binafsi ana uwezo wa kutoa maelezo yaliyojitosheleza.

Katika hatua nyingine Arsene Wenger amezungumzia mchezo wa kesho dhidi ya Stoke City ambapo amesema mchezo huo utakua na upinzani wa hali ya juu kufuatia kila upande kuwa na uwezo wa kiushindani hivyo wao kama wenyeji wanawaheshimu wageni wao ambao kesho watawakaribisha huko Emirates.

Amesema wana matumaini makubwa ya kufanya jitihada ili kufuta makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo uliopita ambao ulishuhudia wakibamizwa bao moja kwa sifuri dhidi ya Man utd ambao walikua nyumbani huko Old Trafford.

Pia akaanika wazi mikakati iliopo sasa ya kuhakikisha wanafanya vyema katika michezo yao ya nyumbani baada ya kucheza na vigogo ugenini kama Chelsea, Liverpool, Man Utd pamoja na Man City.

Nae meneja wa klabu ya stoke City Tony Pulis amesema wanakwenda ugenini hiyo kesho huku wakitambua ugumu na uzuri wa kikosi cha Arsenal ambacho kina wachezaji mahiri ambao wana hamu ya kuitumikia ipasavyo klabu yao baada ya kuanzia benchi kwenye mchezo uliopita dhidi ya Man utd uliochezwa mwanzoni mwa juma hili ambapo wachezaji hao ni kama Fabregas, Denilson pamoja na Robin van Parsie.

Pulis pia amaonyesha kuipiga kijembe Arsenal kwa kueleza wazi kwamba msimu huu imeingia katika mfumo wa vilabu ambavyo tayari vimeshaonyeshwa kadi nyingi nyekundu pamoja na zile za njano, hatua ambayo imeonyesha ni vipi wachezaji wa klabu hiyo wanavyokosa nidhamu wakiwa uwanjani.

No comments:

Post a Comment