Shirika la utangazaji la nchini Uingereza BBC limemtangaza mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ghana pamoja na klabu ya Sunderland Asamoah Gyan kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora ambayo hutolewa kila mwaka na shirika hilo.
BBC wamemtamtangaza mshambuliaji huyo kwenye hafla iliyofanyika jana nchini Misri mjini Cairo usiku wa kuamkia hii leo huku akiwashinda wapinzani wake Andre 'Dede' Ayew, Yaya Toure, Didier Drogba pamoja na Samuel Eto'o ambao walitajwa kuingia katika hatua ya fainali ya kinyanyang’anyiro hicho.
Hata hivyo Asamoah Gyan hakuhudhuria kwenye hafla hiyo kufuatia kubwanwa na harakati za maandalizi ya mchezo wa ligi ambapo kikosi cha klabu yake ya Sunderland jioni ya hii ya leo kilikua uwanjani kikipapatuana na Bolton Wanderres.
Baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa BBC mwaka 2010, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, alitoa shukurani zake za dhati kwa wale wote waliomuwezesha kufikia mafanikio hayo huku akiwalenga zaidi mashabiki wake toka barani Afrika.
Asamoah Gyan, tayari ameshakabidhiwa tuzo yake huko nchini Uingereza ambapo zoezi hilo lilifanyika kwa kumshutukiza huku meneja wa klabu yake Steve Bruce akitumiwa kukamilisha zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment