Meneja wa klabu ya Fulham Mark Hughes ametoa angalizo kwa mameneja wenzake kukaza buti na kuhakikisha wanafikia malengo yaliyowekwa na mabosi wa ngazi za juu kwenye msimu husika wa ligi.
Mark Hughes ametoa angalizo hilo baada ya kuonyesha kuchukizwa na utaratibu unaoendelea kwa sasa ndani ya vilabu vinavyomilikiwa na watu binafsi ambao umekua chanzo cha mameneja kutimuliwa kazi pindi wanapoonekana kushindwa kufika malengo yaliyowekwa.
Amesema licha ya kasumba ya kufukuzwa kazi kwa mameneja kuendelea, bado inaonekana hakuna uwelewa mzuri kwa wamiliki wa vilabu husika ambao mara kadhaa huchukua majukumu ya kuwataka mameneja kuondoka ili hali wameshaviwezesha vikosi vyao kufika katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.
Akitoa mfano wake binafsi pindi alipoondoka huko City Manchester Mark Hughes amesema aliondoka kwenye himaya ya Manchester City huku akiwa tayari amekifikisha kikosi cha klabu hiyo kwenye nafasi ya sita msimu uliopita lakini maamuzi yaliyochukuliwa dhidi yake aliyapokea.
Mark Hughes pia akazungumzia ushirikiano mkubwa alioupata kutoka kwa uongozi wa klabu ya Blackburn Rovers baada ya kuiwezesha klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya sita kwenye msimu wa mwaka 2008-09.
Amesema baada ya kufikia mafanikio hayo uongozi pamoja na wahusika wengine wa klabu ya Rovers walimpa ushirikiano wa kutosha na kumuahidi kuwa bega kwa bega kwenye msimu uliofuata ambao hata hivyo kwa bahati mbaya aliingia mkataba na klabu ya Man City.
Hata hivyo Mark hughes bado anaonekana kuwa kikaangoni kwa sasa kufuatia kikosi chake cha Fulham kuwa kwenye mstari wa kushuka daraja msimu huu.
No comments:
Post a Comment