Meneja mpya wa klabu ya Newcastle Utd Alan Pardew ameendelea na msimamo wake wa kutomuuza mchezaji yoyote ndani ya kikosi chake katika dirisha dogo la usajili.
Alan Pardew ameendelea kutoa msimamo huo, huku akieleza wazi kwamba anafurahishwa na kikosi chake kwa ujumla hivyo anaamini wachezaji waliopo bado wanastahili kuwepo huko St James Park.
Amesema kubwa lililowekwa klabuni hapo ni kuhakikisha wanaendelea kuwa na wachezaji wote kwa kipindi kirefu kijacho kufuatia asilimia kubwa ya wachezaji hao kuwa na umri mdogo.
Hata hivyo mazungumzo hayo yalionyesha kumlenga sana mshambuliaji wa klabu hiyo Andy Carroll ambae siku mbili zilizopita alitangazwa kuhitajika katika himaya ya meneja wa Spurs Harry Redknapp.
Alan Pardew amesema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 siku hadi siku amekua akionyesha kiwango cha hali ya juu hivyo bado msimamo wake upo pale pale wa kutokumuuza.
No comments:
Post a Comment