Meneja wa klabu ya Sunderland Steve Bruce amesema hafikirii suala la kufanya usajili wa wachezaji katika kipindi cha dirisha dogo la usajili kitakachoanza mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka 2011.
Steve ametangaza msimamo huo huku zikiwa zimesalia siku kadhaa kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili ambapo amesema haoni umuhimu wa kufanya hivyo kufuatia kuwa na wachezaji wengi ambao bado anaamini wana uwezo mkubwa wa kumsaidia kwenye kampeni ya kufikia malengo yake msimu huu.
Amesema licha ya kutangaza msimamo wake bado anatambua kuwa yu katika wakati mgumu kufuatia wachezaji wa tano wa kikosi cha kwanza kuwa majeruhi ambao ni Michael Turner, John Mensah,Titus Bramble pamoja na Fraizer Campbell lakini anaamini watarejea kwa wakati muafaka.
Pia akaanisha juu ya mchezaji Lee Cattermole ambae anatumikia adhabu ya kuonyeshwa kadi nyekundu pamoja na mshambuliaji Danny Welbeck aliemsajili kwa mkopo akitokea Manchester United mwanzoni mwa msimu huu, hivyo bado anajiamini kwa kuwa na wachezaji wenye uwazo.
No comments:
Post a Comment