KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 23, 2010

KIBARUA CHA RAFAEL BENITEZ INTER MILAN CHAOTA MAGUGU.


Hatimae uongozi wa klabu bingwa duniani Inter Milan umethibitisha taarifa za kumtimua kazi meneja wa kimataifa toka nchini Hispania Rafael Benitez ambae alijiunga na klabu hiyo miezi sita iliyopita.

Rafa Benitez ameondoka klabuni hapo huku tayari fununu zilikua zimeshaanza kusikika huko na kule kwamba kibarua chake huenda kikaota nyasi lakini uongozi wa Inter Milan ulishindwa kuthibitisha taarifa hizo mapema hususan pindi raisi wa klabu hiyo Massimo Moratti alipokutana na waandishi wa habari mwanzoni mwa juma hili.

Taarifa iliyotolewana uongozi wa klabu ya Inter Milan imeonyesha kumpa baraka zote meneja huyo kuondoka, huku ikimtakia kila la kheri katiak maisha mapya.

Pia uongozi wa klabu hiyo ya nchini Italia umetoa shukurani za dhati kwa Rafael Benitez kwa mema na mazuri aliyoyafanya akiwa huko Guissepe Meaza likiwepo jambo la kuiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa dunia mwishoni mwa juma lililopita kwa kuwabamiza mabingwa wa soka toka barani Afrika TP Mazembe mabao matatu kwa sifuri.

Hata hivyo tayari Rafael Benitez alikuwa ameshaondoka katika himaya ya Inter Millan toka jana na amekua akionekana mjini Liverpool ambapo aliacha amenunu jumba la kifahari na kila alipofuatwa na waandishi kwa lengo la kutaka kueleza kulikoni, alikataa kata kata kuzungumza suala la kuondoka nchioni Italia.

Kurejea kwa Rafael Benitez mjini Liverpool kumeonekana kuwapa nguvu mashabiki wa klabu ya Liverpool ambao hii leo wamesikika wakimpigia upatu meneja huyo ili aweze kurejea kwenye kiti chake ambacho kwa sasa kimekaliwa na Roy Hodgson.

Alipoulizwa Hodgson anajisikiaje juu ya suala hilo, amesema haofii lolote kutokana na kujiamini na kile anachokifanya klabuni hapo, lakini kikubwa kilichomuumiza kwa sasa ni mshtuko wa kutimuliwa kazi kwa Benitez ambae imemchukua miezi sita madarakani.

No comments:

Post a Comment