KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, December 18, 2010

BLATTER AWAPA TANO MAZEMBE.


Raisi wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amewapa tano mabingwa wa soka barani Afrika TP Mazembe kwa kuwa klabu ya kwanza kutoka barani hapa kutinga kwenye hatua ya fainali ya klabu bingwa duniani.

Blatter ametoa pongezi hizo kwenye mkutano wa mwisho na waandishi wa habari kabl ya kucheza kwa hatua ya fainali ya michuano ya klabu bingwa duniani ambapo hii leo mabingwa wa barani Ulaya inter Milan wataonyeshana kazi na Tp Mazembe huko mjini Abu Dhabi.

Blatter amesema hana budi kutoa pongezi hizo kwa klabu hiyo, kufuatia soka safi walilolionyesha toka walipoanza mikakati ya kutinga kwenye hatua ya fainali na anaamini hiyo ni ishara nzuri kwa bara la Afrika kuendeleza hatua za kukuza soka lake.

Amesema TP Mazembe wametengebneza historia mpya duniani ambayo inawathibitishia wazi wale waliokuwa wakiibeza Afrika siku za nyuma na hii leo, kwa hakika watakua wakizihofia klabu za barani humo pamoja na timu za taifa pale watakapokutana nazo kwenye michuano ya kimataifa na hata kwenye michezo ya kimataifa ya kirafiki.

Mbali na kutoa pongezi hizo, mzee huyo mwenye umri wa miaka 73, pia akatoa angalizo kwa vilabu vingine vya barani Afrika kuhakikisha vinaweka mipango mizuri na madhubuti ambayo itaviwezesha kufikia hatua kama ilivyo kwa TP Mazembe ambao ni mabingwa mara mbili mfululizo wa barala la Afrika.

TP Mazembe imekua klabu ya kwanza kutoka barani Afrika kufika hatua ya fainali ya michuano ya klabu bingwa duniani toka ilipoanzishwa mwaka 2001.

No comments:

Post a Comment