Meneja wa klabu ya Aston Villa Gerard Houllier amekataa kata kata kuwa tayari kumruhusu winga wake wa kimataifa toka nchini Uingereza Ashley Young kuondoka katika kipindi cha usajili cha mwezi januari.
Gerard Houllier amekataa kutoa nafasi hiyo badaa ya Ashley Young mwenye umri wa miaka 18 kuhusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu ya Liverpool pamoja na Tottenham Hotspurs.
Amesema Ashley bado yupo kwenye mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo ya mjini Birmingham hivyo ameusisitiza uongozi wa ngazi za juu kutomuweka kwenye orodha ya wachezaji watakaouzwa katika kipindi cha usajili cha mwezi Januari mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment