KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, December 22, 2010

BIG SAM NAE AFUNGUKA !!


Siku kadhaa baada ya uongozi mpya wa klabu ya Bluckburn kutoa sababu za kumtimua aliekua meneja wa klabu hiyo Sam Allardyce, meneja huyo nae ameibuka na sababu zake ambazo amedai zilipelekea kufukuzwa kazi huko Ewood Park.

Sam Allardyce ambae kwa sasa yupo nyumbani huku akisubiri bahati ya mtende imuangukie ili aweze kupata nafasi ya kukinoa kikosi cha klabu yoyote itayomuhitaji amekanusha taarifa zote zilizotolewa na mwenyekiti wa Bluckburn Rovers ambazo zilidai meneja huyo alitumiliwa kazi baada ya kushindwa kuweka bayana mikakati ya kuiendeleza klabu hiyo kwa kuwa na vikosi vya wachezaji chipukizi.

Sam Allardyce mwenye umri wa miaka 56 amesema ukweli ni kwamba wamiliki wapya wa klabu hiyo walimtaka kufuata utaratibu wao wanaona ni bora zaidi yake yeye kama meneja, na mwisho wasiku walishindwa kukubalina utaratibu huo na kujikuta wakishindwa kufikia muafaka.

Amesema yeye kama meneja wa muda mrefu ambae tayari ameshapita katika nafasi mbali mbali anajua nini anachokifanya anapokua kwenye majukumu yake ya kikazi hivyo ni kitendo cha aibu kufundishwa ni vipi anavyotakiwa kufanya kazi kwa malengo ya kupata mafanikio.

Sam Allardyce bado akaendelea kubainisha kwamba yeye hakuwa mpuuzi wa kufanya kazi kila juma, kila mchezo, kila msimu na kila mwaka kwa kuhakikisha kikosi chake kinafikia mafanikio aliyojiwekea hivyo bado alistahili kuheshimiwa.

Wakati huo huu uongozi wa klabu ya Blackburn Rovers umeendelea kushikilia msimamo wake wa kumtumia meneja msaidizi Steve Kean hadi mwishoni mwa msimu huu wakati ukiendelea na mchakato wa kumsaka mrithi wa Big Sam.

Kean, mwenye umri wa miaka 43, tayari ameshaitumikia kazi yake kama meneja wa muda wa Rovers mwishoni mwa juma lililopita na alifanikiwa kupata matokeo ya sare ya bao moja kwa moja dhidi ya West Ham Utd.

Hata hivyo tayari Steve Kean ameshatangaza hadharani kuitaka kazi ya umeneja klabuni hapo kwa kujipigia upatu kupitia uzoefu wa miaka tisa alioupata akiwa huko Ewood park.

Hatua hiyo ya Steve Kean kuomba nafasi ya umeneja klabuni hapo imepingwa vikali na Sam Allardyce ambae amesema meneja huyo wa muda hana uwezo wa kutosha wa kufikia malengo yalitowekwa na viongozi wapya wa klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment