Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Cameroon pamoja na klabu bingwa duniani Inter Milan Samuel Eto'o usiku wa kuamkia hii leo alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora barani Afrika kwa mwaka 2010.
Eto’o ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo kwenye hafla maalum iliyoandaliwa na shirikisho la soka barani Afrika, huko mjini Cairo nchini Misri.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29, amefanikiwa kuwa mchezaji bora wa bara la Afrika huku akiwabwaga wapinzani wake aliongia nao kwenye hatua ya fainali ambao ni mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ghana Asamoah Gyan pamoja na mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ivory Coast Didier Drogba.
Hii inakua ni mara ya nne kwa Samuel Eto’o kutwaa tuzo hiyo ambapo kama inakumbukwa vyema amewahi kutwaa tuzo hiyo mara tatu mfulizo na hiyo ilikua mwaka 2003, 2004 pamoja na 2005 kipindi ambcho alikua kiitumikia klabu ya Barcelona ya nchini Hispania.
Kwa mafanikio hayo Eto’o anavunja rekodi iliyowekwa na magwiji wa soka barani Afrika ambao ni Abedi Pele pamoja na George Weah ambapo kila mmoja wamewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora mara tatu.
Baada ya kutangazwa kuwa mshindi, mshambuliaji huyo alitoa shukurani zake za dhati kwa aliekua meneja wake Jose Mourinho ambapo amedia ana imani kubwa meneja huyo wa kimataifa toka nchini Ureno amefanikisha mafanikio aliyoyapata msimu uliopita na huu uliopo sasa.
Pia akamshukuru meneja wake wa sasa Rafael Benitez kwa kuendeleza mazuri aliyoyaacha Mourinho huko Inter Milan na bado akaendelea kusisitiza kwamba suala hilo nalo limechangia yeye kuibuka mshindi barani kwake.
Kwa upande wa tuzo ya kocha bora barani Afrika, Milovan Rajevac aliekua na jukumu la kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Ghana katika fainali za kombe la dunia alitangwzawa kuwa mshindi wa tuzo hiyo huku akimbwaga kocha wa klabu ya TP Mazembe Lamine N'Diaye pamoja na kocha wa kikosi cha timu ya taifa ya Misri Hassan Shehata.
Kojo "Kwadwo" Asamoah kiungo mdogo wa kimataifa toka nchini Ghana yeye ametangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa bara la Afrika mwenye umri mdogo huku akiwashinda wapinzani wake Ryad Boudebouz (Algeria) pamoja na Moussa Maazou (Niger).
Mkongwe na nahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya Misri Ahmed Hassan mwenye umri wa miaka 35, yeye ametangazwa kuwa mchezaji bora wa bara la Afrika alidumu kwa muda mrefu.
Tuzo ya klabu bora barani Afrika imekwenda kwa mabingwa wa barani humo pamoja na washindi wa pili wa dunia TP Mazembe kutoka jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
Nae Mwanadada Perpetua Nkwoche yeye ametajwa kuwa mchezaji bora wa kike wa bara la Afrika.
No comments:
Post a Comment