KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, December 22, 2010

FIFA YATOA TAMKO LA KUMTAMBUA BWALYA !!


Mkutano maalum ulioushirikisha ujumbe wa watu sita kutoka nchini Zambia pamoja na maafisa wa shirikisho la soka duniani FIFA umefanyika huko mjini Zurich nchini Uswiz huku muafaka ukitangazwa kupatikana.

Mkutano huo ulioombwa kufanyika baada ya raisi wa Zambia Rupia Banda kukutana na Sepp Blatter na kumuomba usaidizi wa kumaliza mgogoro wa soka unaoendelea kati ya raisi wa chama cha soka nchini Zambia Kalusha Bwalya dhidi ya wadau wa mchezo huo nchini humo.

Muafaka uliopatikana kwenye mkutano huo wa siku ya jumatatu ya juma hili, unaendelea kumuidhinisha raisi wa sasa wa chama cha soka nchini Zambia Kalusha Bwalya kuendelea na wadhifa wake, kufuatia uongozi wa FIFA kutoa kauli ya kumtambua kiongizi huyo ambae bado hajamaliza muda wake.

Hata hivyo maafisa wa FIFA wameushauri ujumbe huo wa watu sita uliotumwa na raisi Banda kurejesha ujumbe nchini Zambia ambao unatoa haki ya kidokrasia kwa kamati ya utendaji ya chama cha soka nchini humo kupiga kura ya kutokua na imani na kiongozi huyo pindi kamati hiyo itakapokutana mwezi March mwaka 2011, hatua ambayo itathibitisha ni vipi kiongozi huyo asivyoamiwa na viongozi wengine.

Kurejeshwa kwa ujumbe huo mara baada ya kikao hicho kilichofanyika siku ya jumatatu, kumeonekana kupokelewa vyema huko nchini Zambia hatua ambayo imemfanya raisi wa nchini Zambia Rupia Banda kulishukuru shirikisho la soka duniani FIFA kwa ushauri uliotolewa ambao anaamini utakuwa jibu la kusuluhisha zogo linaloendelea nchini kwake kupitai mchezo wa soka.

Kalusha Bwalya kwa muda sasa amekua kwenye wakati mgumu wa kupingwa na viongozi wenzake wa chama cha soka nchini Zambia ambao wanadai, kiongozi huyo amekua anakwenda kinyume na utaratibu wa madaraka yake hali ambayo imekua ikizua tafrani kila kukicha ndani ya mchezo wa soka nchini humo.

No comments:

Post a Comment