KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, December 17, 2010

BLATTER AWAOMBA RADHI MASHOGA !!


Baada ya raisi wa shirikisho la soka nchini duniani FIFA Sepp Blatter kutakiwa kuwaomba radhi mashoga wote ulimwenguni kufuatia kauli yake aliyoitoa nchini Afrika kusini mwanzoni mwa juma hili, hii leo raisi huyo amelazika kufanya hivyo.

Blatter amelazimika kuomba radhi kupitia mkutano na waandishi wa habari huko mjini Abu Dhabi baada ya kuulizwa ni vipi ameichukulia changamoto hiyo iliyotolewa na mchezaji wa zamani wa mchezo wa mpira wa kikapu toka nchini Uingereza John Amaechi ambae ameshajitangaza hadharani kuwa ana tabia za ushoga.

Blatter amesema changamoto hiyo aliipokea kwa mikono miwiwli na ifahamike kuwa kauli aliyoitoa dhidi ya mashoga huko nchini Afrika kusini haikuhusiana na ubaguzi kama ilivyodaiwa John Amaechi siku mbili zilizopita.

Hata hivyo mzee huyo mwenye umri wa miaka 74, amewataka radhi mashoga wote ulimwenguni kwa kauli aliyoitoa ambayo ana imani kubwa imewauma.

Lakini pamoja na kuomba radhi, bado sheria za umoja wa nchi za falme za kiarabu zinawabana mashoga kufanya vitendo vyao wakiwa ndani ya nchi hizo sambamba na unywaji wa pombe.

No comments:

Post a Comment