KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, December 18, 2010

GRANT ASEMEA AHOFII KUFUKUZWA KAZI !


Meneja wa wa klabu ya West ham Utd Avram Grant amesema hafikirii kutimukliwa kazi klabuni hapo bali anachokifikiria kwa sasa ni kuhakikisha anairejesha klabu hiyo katika utaratibu wa kupata point tatu muhimu na kuondoka kwenye mstari wa kushuka daraja msimu huu.

Avram Grant ametoa msimamo huo baada ya saa kadhaa kupita ambapo uongozi wa klabu hiyo ulimtaka kuhakikisha anashinda michezo mitatu mfululizo na endapo atakwenda kinyume na maagizo hayo atapoteza kibarua chake.

Amesema amekua akijitahidi kila kukicha kufanya mipango madhubuti ya kutimiza malengo hayo lakini changamoto wanazokutananazo zinawauwia vigumu hivyo ana kwa sasa anasaka mbinu mbadala ambazo zitamuwezesha kunya vizuri.

Avram Grant ambae badoa naklumbukwa kwa kuiwezesha Chelsea kutinga kwenye hatua ya fainali ya ligio ya mabingwa barani ulaya msimu wa mwaka 2007-08 pia ameeleza wazi kwamba kikosi chake mara zote kimekua kikionyesha mchezo mzuri zaidi ya wapinzani wao lakini kimekua hakina bahati ya kumaliza dakika 90 bila ya kuwa na point tatu muhimu.

Kikosi cha West Ham Utd kwa sasa kinashika nafasi ya 20 kwenye msimamo wa ligi huku kikiwa kimeshajikuzanyia point 12.

No comments:

Post a Comment