Meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Ancelotti amesema anaamini cmhezo wa kesho dhidi ya man utd utakua na mvuto wa upinzani kufuatia pande zote mbili kuwa na malengo ya kuendelea kuwepo katika kinyanganyiro cha nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi.
Anceloti amesema mchezo huo utakuwa katika hali hiyo kufuatia wapinzani wao kuwa na hali ya kujiamini kupita kiasi baada ya kushinda mchezo uliopita dhidi ya Arsenal na kufanikiwa kurejea kileleni kwa kufikisha point 34.
Amesema kutokana na hali hiyo tayari wao wameshajiandaa vya kutosha kuhakikisha hawaendelezi kasumba ya kupoteza point kama ilivyokua kwenye michezo iliyopita ambapo ushindi wao ulikuwa sare.
Hara hivyo Anceloti akatoa angalizo kwa wapinzani wao Man Utd kwa kuwaeleza kwamba wasidhani tayari wameshakihakikishai ubingwa baada ya kufanikiwa kurejea kileleni, kwani kindumbwe ndumbwe cha kusakaubingwa bado kinaendelea kwa vilabu vingine.
Wakati huo huo meneja wa klabu ya man utd Sir Alex Ferguson nae amezungumzia mchezo huo wa kesho hukua kionyesha kutambua ugumu wa wapinzani wao ambao watakua nyumbani huko Old Trafford.
Amesema anakwenda jijini London akiwa na kikosi kamili tena chenye kujiamini lakini bado anahofia ugumu wa Chelsea ambao wana rekodi nzuri ya kutopoteza mchezo kirahisi wanapokua kwenye uwanja wao wa nyumbani.
No comments:
Post a Comment